Ssemakula

Mzee wa miaka 94, wake 19 na watoto 100 aoa tena, kunani ?

Mzee Nulu Ssemakula, raia wa Uganda mwenye miaka ya zaidi 94 na wanawake zaidi ya 19 amezua gumzo kwa kuongeza familia yake kwa kuoa wake wanne tena.

Hata ingawa baadhi ya watoto wake wana wajukuu, mzee huyu anasema bado ana matumaini ya kuwa na watoto zaidi na hata wake wengi zaidi.

Mzee huyu ambaye  alianzisha shule yake binafsi kwa madhumuni ya watoto ambao ni  zaidi za 100.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Ssemakula alielezea kuwa matamanio yake ya maisha ni kuwa na wake  na watoto  wengi kwanikama familia yake kubwa ikitafsiriwa kwa utajiri.

Mwanahabari Aliyekejeli Ushindi Wa Kipchoge Akemewa Mtandaoni

“Kwa bahati mbaya, nimepoteza wake wangu wanne na wengine ambao wanahitaji zaidi ya uwezo wangu, niliwaacha waende. Lakini waliniachia watoto; Bado nitaoa zaidi ikiwa bado nina miaka zaidi na hata nina watoto zaidi. Katika watoto na wake, ndipo ninapopata raha yangu. Huo ni utajiri wangu wa kweli, “alisema.

Kwa sasa, Ssemakula anaishi na watoto wake 66, mdogo zaidi akiwa na miezi 10. Mkewe wa mwisho ana miaka 24 na anatazamia kuongeza familia yake zaidi.

Ssemakula alianzisha shule iitwayo Kiyombero Shule ya Msingi ili kuwakidhi watoto wake wote wanaoenda shule na wajukuu.

Rais Mtaafu Moi alazwa katika Nairobi Hospital

Shadiah Tumuheirwe, mkewe ambaye ni mdogo kwa wote, ni kiongozi. Yeye hupeana maagizo na masharti katika familia.

Mbali na kujenga shule, Ssemakula anamiliki mashine ya kusaga kahawa na nyinginr ya kuhifadhi maziwa kama kitega uchumi na kuleta mapato kwa ajili ya kuimudu familia yake.

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments