'Mziki wetu haumdhuru mtu yeyote' Familia ya Ochungulo yajibu

Wanamziki wa kikundi cha Ochungulo ambao kwa lugha ya Luo inamaanisha mchwa, wamesema kwamba muziki wao haudhuru mtu yeyote.

Familia hii ambayo imeundwa na Nelly, Benzema na Dmore walianza maisha ya mziki kibinafsi mwaka wa 2017, 2012 na 2015 kwa mpangilio.

Katika mahojianao yaliyoskika na radio jambo Ochungulo walisema waliamua kutumia jina  hilo kwa sababu wakati wanakuja pamoja wanatengeneza miziki mizito na wakuvutia umati mkubwa sana.

Kufanya kazi na the Kansoul wamesema ilikuwa ni nafasi yao ya kujielimisha.

Wamekuja na jina la mziki ambazo wanafanya na wanaliita, Gengeton. Wanasema ni kwa sababu wasanii kama vile Juacali aliyefanya Genge ni motisha kwao hivyo wanataka  kuendeleza mahali waliachia.

Familia ya Ochungulo inasema wanaporekodi video zao huwa hawafikirii kama nyimbo zao zita pigwa marufuku kwa jina la maudhui kwa kuwa hawatoi mziki ambayo inadhuru mtu papo hapo.

Hakuna hali yoyote ya matusi kwa mtu kwa sababu wanaimba kitu ambacho tayari kiko.

Kitu kinacho wapa muskumo ni sababu mziki ni kila kitu kwao.

Hatutawacha kwa lolote. Bado tutawapa wakenya miziki mizuri ata kama watu wanao tupigia debe hawatulipi. Wanatudhania kama watoto lakini tumejifunza. Sasa tuna masharti makali.

Walipoulizwa kama wana tashwishi kuwa wazazi wao huona mziki wao walisema ndio na wazazi wao wanawafuata kwenye chaneli yao.

Kulikuwa na matatizo mwanzoni walipohisi kuwa walikuwa wanatumia maneno mengi kwa nyimbo zao ambazo hazina maudhui lakini baada ya kuwashawishi waliona kuwa mashabiki wao wanapenda mziki wao hivyo wakawa na furaha.

Burudika na wimbo wao mpya Aluta.