Gregory Dow, 61, alikubali kwamba alitejeleza maovu hayo kati ya mwaka wa 2013 na 2017 katika kituo hicho ambacho yeye na mkewe walikuwa wakikiendesha .
Chini ya makubaliano na upande wa mashtaka ,Dow atahukumiwa miaka 15 na miezi minane jela .Atahukuiwa rasmi septemba tarehe 29.
Dow anadaiwa kuwadhulumu wasichana hao wakati wawili kati yao walipokuwa nanumri wa miaka 11 ,mmoja miaka 12 na mwingine alikuwa na umri wa miaka 13
Dow alijifanya kuwa mhudumu wa kimishenari wa kikristu a kuanzisha kituo cha kuwahudumia mayatima na badala yakuwatunza kama baba alianza kuwadhulumu kimapenzi .
Alitumia nguvu ili kutekeleza dhulma hizo kwa mujibu wa waendesha mashtaka katika kesi hiyo .
Kituo hicho cha Dow cha utunzi wa watoto kilichoanzishwa mwaka wa 2008 huko Boityo kilifungwa mwaka wa 2017
Maamlaka za Kenya zilijaribu kumkamata Dow mwaka wa 2017 lakini alifaulu kutoroka na kurejea marekani .
Maafisa wa FBI na polisi wa eneo alikokuwa walifaulu kumanasa na kumkamata julai mwaka wa 2019