Nafurahi bwanangu aliaga dunia, nilizika stress - Jessica

Katika kipindi cha Bustani la Massawe, bi Japanni aliamua kuanzisha mjadala na waskizaji wake ambao ni wajane.

Katika majadiliano hayo, alitaka kujua kama kuna wajane ambao tayari wameingia kwa ndoa zingine au wameamua kuendelea na maisha kivyao.

Katika harakati hiyo, mwanadada mmoja kwa jina Jessica aliwashangaza wengi alipokiri kuwa licha ya kubaki mjane na mama wa watoto wasio na baba, anafurahia kuwa mumewe aliaga dunia.

Kulingana na Jessica, hakuzika mumewe tu lakini alizika stress!

Katika usimulizi wake, mwanadada huyo alifunguka jinsi mumewe alikuwa anampiga mbele ya wanao wachanga na kumpa mateso ya kimawazo.

Jessica bila aibu alisema kuwa tangia kifo cha mumewe mwaka wa 2016, afya yake imenawiri na ameongeza kimo. Alisema kuwa hata mumewe akaamka sasa hivi atashindwa kumtambua.

Kwa kile alichopitia, Jessica alikiri hayuko tayiri kuingia kwa ndoa nyingine na heri aishi pekee yake na watoto wake.

Soma usimulizi wake,

Aii hiyo maisha ya kwenda kutafuta ndoa ingine ni magumu, mume wangu aliaga dunia mwaka wa 2016 na hiyo mambo ya kuingia kwa ndoa mara ya pili na mtu akupee stress.

Yalikuwa maisha magumu na hata sahii nahisi nimepumzika, mungu alikuwa tu na sababu juu hata ilifika kiwango chetu kuwachana. Nakuambia sahii hat watu wanashangaa ni mimi kweli juu hata akiamka sahii atashangaa sio mimi.

Alikuwa mwanaume sumbua tu yaani. Nakuambia si nimekula viboko mwili wangu sahii hata sipendi mtu akiniguza ni uchungu tu. Watoto wako tu wako sawa na mpaka wammiss baba yao kwani aliwaacha wakiwa wachanga.

Nilifika mahali hadi nikasema hata heri mwenye amezika, wacha niishi maisha ya upweke lakini sina hiyo stress, mimi stress pekee ingeniua ningekufa kama tu nimeketi.