'Nahodha Granit Xhaka anafaa kuomba msamaha,' - Unai Emery

xhaka
xhaka
Kocha wa Arsenal Unai Emery amesema Granit Xhaka anafaa kuomba radhi baada  kuonekana kujibizana na mashabiki wa kilabu hiyo  wakati wa mchuano waliotoka sare ya mabao mawili na Crystal palace siku ya jumapili.
Hatua hiyo iliwapelekea mashabiki kumkemea nahodha huyo wa The Gunners.

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amewaunga mkono wachezaji Fred na Andreas Pereira kuziba pengo la safu ya kati lililoachwa wazi na mchezaji anayeuguza jerala Paul Pogba. Pogba hajacheza tangu septemba tarehe 30 na huenda akawa nje ya uwanja hadi Disemba kwa ajili ya jeraha la mguu.

Mshambuliaji wa wales Gareth Bale hajawahi kuzungumza kuhusu kuondoka Real Madrid, amesema kocha Zinedine Zidane. Bale, mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kujiunga na kilabu ya uchina Jiangsu Suning lakini uhamisho huo ukafeli.

Bulgaria imeagizwa kucheza mechi mbili bila mashabiki uwanjani huku mchuano mmoja ukitarajiwa kuchezwa baada ya miaka miwili kwa hatua ya mashabiki wake kuwatukana wachezaji weusi wa England wakati wa mchuano wa kufuzu kwa kombe la Euro mwaka ujao.

England ilishinda Bulagria mabao sita kwa nunge huko sofia katika mechi ambayo nusra isitishwe iwapo wachezaji wa England hawangeamua kuimaliza.

Tukirejea nchini, mchezaji wa kikosi cha raga cha Sevens  Collins Injera  atakosa mchuano wa kufuzu kwa  mechi za olimpiki mwaka ujao mjini Tokyo uliopangwa kusakatwa kati ya novemba tarehe 8 hadi 9 nchini afrika kusini.

Hata hivyo maneja wa timu Eric Ogweno  amethibitisha kwamba Injera aliyejeruhiwa bega wakati wa mechi za safari sevens atakuwa katika hali nzuri kushiriki mechi za msururu wa IRB msimu wa 2019/2020 mwezi disemba.