Nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama kujiunga na Bournemouth?

Kocha mkuu wa Bournemouth, Eddie Howe sasa ananuia kumsajili kiungo wa Tottenham na nahodha wa Kenya, Victor Wanyama. Spurs are

Kulingana na jarida la The Sun, Spurs wanapania kuleta fedha zaidi ili kumwezesha kocha Mauricio Pochettino's kusajili wachezaji zaidi.

Baada ya ujio wake Tanguy Ndombele kwa kitita cha pauni milioni 65, timu hiyo ya North London sasa inanuia kumuuza Wanyama.

Wanyama alimfuata Pochettino kutoka Southampton hadi Tottenham kwa pauni millioni 11.5m mwaka wa 2016.

Kulingana na Daily Mail, Spurs wanapania kutengeneza ingali kiasi walichomsajili nacho huku West Ham na Galatasaray ya Uturuki zikionesha hamu ya kumsajili.

 

Wanyama, 28, alilazimishwa kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kombe la Audi ambacho walishinda baada ya kukumbwa na jeraha la goti.