Nahodha wa zamani wa Harambee Star Musa Otieno aondoka hospitalini

M O
M O
Aliyekuwa kapteni wa timu ya taifa ya soka Harambee Star Musa Otieno ameruhusiwa kwenda nyumbani kutka hospitalini .

Otieno amekuwa  katika hospitali kuu ya KNH  kwa siku 10   akipokea matibabu kwa  maradhi yenye dalili kama za virusi vya corona. Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 46  amemshukuru Mola na wote waliomtakia afueni ya haraka alipokuwa kitandani.

Amesema hali yake imeboreka lakini atalazimika kujitenga kwa siku 14 zaidi  kama inavyotakikana na wizara ya afya.