Najua Ben Githae ana watoto sita nje ya ndoa - Rose Wanjiru

rose.wanjiru
rose.wanjiru
Rose Wanjiru ni mwanamke ambaye alijitokeza akidai kuwa alikuwa na uhusiano na msanii Ben Githae kwa miaka mitano.

Katika uhusiano wao, wawili hao walijaliwa na watoto wawili wa kike ambao ni mapacha.

Hata hivyo shida kati yao ilianzia wakati Rose alimfahamisha Githae kuwa ni mja mzito na anadai kuwa msanii huo wa 'Timiza' alimshauri aavye mimba hiyo. Alipokataa kufanya hilo, Githae alimtumia wanaume ili wamuue.

Juzi katika mahojiano na Massawe Japanni, Githae alijitetea akisema kuwa ana mke wa miaka kumi na minane na kuwa yeye na Rose walikuwa tu marafiki.

Alidai kuwa Rose ndiye aliyemtishia maisha ndiposa aweze kumfanyia mambo ama afichue siri kwa vyombo vya habari.

“Rose aliweza nitishia maisha ili nimfanyie mambo kadhaa na nisipomfanyia alikuwa ananiambia ataweza kuambia vyombo vya habari kuwa ako na mtoto na mimi,” Ben alizungumza.

Hata hivyo, Rose alifichua kuwa wawili hao walikuwa kwa uhusiano wa miaka mitano kuanzia 2011 hadi 2016 na kwamba hakuwa na habari kuwa mwanamuziki huyo alikuwa na bibi.

Alisema kuwa Githae alimwambia kuwa alikuwa ametengana na mkewe na kutoka hapo wawili hao walikuwa wanapatana katika mikahawa kadhaa Nairobi. Alieleza kuwa msanii huyo alikuwa anajificha uso kila mara wakipatana.

Kando na wanawe wawili, Rose anakiri kuwa ana uhakika kuwa Ben Githae ana watoto wanne zaidi nje ya ndoa na kuwa mmoja wa wanawake yupo tayari kujitokeza.

Nina uhakika kwani mmoja wa wanawake alisema kuwa atajitokeza baada yangu kujitokeza. Aliniambia Ben ana watoto sita nje ya ndoa ukihesabu wangu wawili.

Huyu mwanamke alipata nambari yangu ya simu kupitia Ben ambaye alimpatia akimshawishi anitusi na hapo ndipo alinifungulia roho. Alieleza Rose.

Soma usimulizi wake.

From 2016 wakati nilibeba mimba, nilimjulisha nina mimba yake ikiwa ya miezi mitatu. Hapo aliniambia niavye mimba na nikakataa, alinitumia watu wakanipiga na nikalazwa hospitalini kwa mwezi mmoja.

Wakati mimba yangu ilifikia miezi saba nilitolewa hao watoto juu ya shida nilizipata.

Hauamini kuwa uliingilia ndoa yake?

Yeye mwenyewe aliniambia kuwa ametengana na mkewe na sikufuatilia.

Una uhakika upi ni yeye alikutumia wale watu?

Nina uhakika juu walikuwa wananipigia simu wakija kunitafuta Thika kupitia mwanamke. Sasa alikuwa akiniuliza kwenye mimi husongwa nywele na nilipomwelezea alidai kuwa stima zimepotea. Hapo akaanza kunilazimisha kuwa anataka kujua ninakoishi.

Kuna siku nilienda kumtafuta Ben katika hoteli ya Blue Springs kwani sikuwa naweza kujilipia kodi ya nyumba. Kumpigia simu hakuwa anajibu na wanaume wawili wakaniambia tuondoke twende katika hoteli nyingine.

Tulipofika Ngara, hao wanaume wakashikana wakawa wanne. Kuna venye walikuwa wananidanganya ili niingie mahala kuna giza na nikakataa na kurudi Blue Springs.

Pale Blue Springs, Ben hakutaka kuzungumza nami ila alinizaba kofi moja huku wale wanaume wakiwa nyuma yangu. Alitoka akaenda na akwacha nikipigwa na wale walinzi hawakunitetea.

Baadaye, Ben Githae alienda na kuripoti Kasarani kuwa nimempiga nami nikamripoti lakini siku ambayo tulikuwa tupatane hakufika na hayo mambo yakaisha.

Baada ya kupigwa, Ben alisafiri hadi marekani kwa mda wa miezi miwili na alirudi nikikaribia kujifungua. Wakati nilikuwa na shida kadha wa kadha aligharamia fedha za hospitali lakini hakuja kuwapokea watoto.

Nini ilikusukuma kwenda katika vyombo vya habari?

Kitu kilinisukuma ni kuwa nilikuwa natishiwa maisha na wanawake ambao walikuwa wanasema kuwa wanajua uhusiano wangu naye na kuwa wanajua ninakoishi.

Nikimweleza anasema sio yeye aliye watuma.

Ushauri kwa wanawake walio katika mipango ya kando

Mipango sio mbaya ila mwanaume akileta ujinga unajitokeza.