'Najuta kuwa 'Bully' Irungu Kangata amwambia Jacque Maribe

FB_IMG_1597604410416
FB_IMG_1597604410416
Katika sekta yake ya kuchambua siasa katika kipindi kinachofahamika kama 'the hot seat'mwanahabari Jacque Maribe alikuwa katika mahojiano na kiranja wa wengi katika seneti Irungu Kang'ata.

Kiranja huyo alisimulia maiisha yake akiwa katika sule ya upili na kusema,

"Najutia mambo mengi ambayo nilitenda nilipokuwa katika shule ya upili sana sana Bullying, ulikuwa utamaduni wa shule nakumbuka viendo na mambo ambayo tulikuwa tunawaambia wanafunzi wa kidato cha kwanza waweze kufanya
Kama ningeweza rudisha wakati nyuma ningekuwa katika mstari wa mbele kupigana dhidi ya vitendo hivyo, lilikuwa jambo au vitendo vibaya katika shule ya upili ya Thika." Aliongea Kang'ata.

Mwaka wake wa kwanza na wa pili hakupata alama njema katika mitihani yake, huku siku moja akifukuzwa shuleni ambapo alibadili mawazo yake kuhusu shule.

"Nilianza  kumwandikia mwalimu mkuu barua nikimwambia kuwa tunataka chai mwendo wa saa nne, niliandika jumbe nyingi mpaka siku moja shule iliamua kufanya uchunguzi nani haswa anaandika barua hizo

Ningeziandika na kisha kuzipeleka katika ofisi ya mwalimu mkuu bila yake ya kujua wala kufahamu."

Irungu alisema kuwa alipenda nyimbo za raggae akiwa katika darasa la sita na kupenda siasa akiwa darasa lilo hilo.

"Upendo wangu kwa nymbo za Raggae ulianza nikiwa katika darasa la sita na hata hamu ya siasa ilianza nikiwa darasa la sita, ilifika mahali nikiwa chuo kikuu nilifukuzwa kwa maana nilianza kucheza deki yaani kua DJ."

Alidokeza kkuwa alipenda muziki kwa sababu ya ndugu zake wakubwa