Najuta!! Natamani ningekuwa makini maishani nikiwa mdogo- DJ Mo

Kila mmoja wetu lazima ajute kwa jambo au tendo ambalo alifanya hapo awali, na kutamani angekuwa na uwezo kurudisha wakati nyuma.

Akiwa katika mahojiano DJ Mo alisimulia majuto yake makuu katika maisha yake, huku akisema angelipewa muda arudi awe na miaka,15, angerekebisha makosa yake na kufanya maisha yake yawe bora.

"Ndio ninajuta sana katika maisha yangu natamani ningeanza kuwa mwangalifu na kuanza kufanya kazi nikiwa na miaka,15,

Wakati ambao niligundua napaswa kuwa makini maishani nilikuwa na miaka 26/27, watu wengi hungoja kufikisha miaka, 27 ili wawe waangalifu na maisha yao

Nakungoja tena hadi miaka thelathini ili waokoke, natamani ningeanza kutafuta riziki nikiwa na miaka kumi na tano." Mo Alieleza.

DJ Mo aliendelea na kusema kuwa kwa sasa yupo sawa na pesa anazo, hajuti kumpa mwanawe Ladasha chochote anahitaji maishani.

" Huwa nampa chochote ambacho nahitaji, kwa maana sikuwa na hivi vitu utotoni, Akiuliza kitu leo mimi humpa kesho.

Hii ni kwa sababu nafanya kazi ili niweze kumpa anachohitaji maishani." Aliongea.

Alipoulizwa atakacho mpa mwanawe Ladasha alikuwa  na haya ya kusema,

"Kitu ambacho naweza kumpa kwa sasa ni neno la Mungu kwa maana ukimfunza kila kitu chochote kitakuwa mahali kinapaswa kuwa." Alizungumza DJ Mo.

DJ Mo na mkewe Size 8 wamefungua biashara ya kuosha magari na duka la ulimbwene.