eliud kipchoge and tottenham hotspur players

Nakuamini!! Wanyama amtakia Eliud Kipchoge heri njema

Mwaka wa 2018, bingwa wa nyimbo za nyika na anayeshikilia rekodi ya mbio hizo, Eliud Kipchoge alikuwa na wakati wa kufana mno.

Hii ni baada ya mkenya mwenzake Victor Wanyama anayechezea timu ya Uingereza, Tottenham Hotspurs pamoja na wafanyikazi wa klabu hiyo walimlaki na kumpa ziara njema katika makao makuu ya timu hiyo, jijini London.

[PICHA] Maandalizi ya Kipchoge Vienna kabla ya Ineos1:59 Challenge

Ziara ya Kipchoge ilijia siku chache tu baada ya kushinda mbio za nyika mjini London, kwa mara nyingine tena.

Katika ziara hiyo, Kipchoge na Wanyama walipiga picha pamoja kabla yake kupiga na wachezaji wengine na kocha Mauricio Pochettino.

Mwaka uliopita, bingwa huyu alikuwa katika mstari wa mbele huku akimtakia Wanyama na timu yake ushindi katika fainali za kombe la mabingwa wa ulaya.

Hata hivyo, leo ilikuwa zamu yake nahodha huyo wa Harambee Stars kumtakia Kipchoge heri njema, anapojitayarisha kuivunja rekodi ya mbio za nyika zijulikanazo kama INEOS 1:59 challenge.

Video: Eliud Kipchoge backs Tottenham to beat Man City tonight

Mbio hizo ambazo zitafanyika jijini Vienna, zimefadhiliwa na bwanyenye wa Uingereza, Sir Jim Ratchliffe.

 

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Wanyama alichapisha picha yake pamoja na Kipchoge huku ujumbe wake ukisoma,

Let me take this earliest opportunity to wish my friend and countryman, @kipchogeeliud the best in the “INEOS 1:59 Challenge” in Vienna Austria this Saturday.

I believe you in your capability will run that marathon in 1:59 bro 💪🏾

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments