dennis.and.mariga

Nakutakia siku njema ya wapendanao Itumbi amwambia Jowie

Dennis akiwa katika mahojiano na runinga moja nchini alieleza uhusiano wake na Jacque Maribe, na kumkaribisha Jowie baada ya kuachiliwa na kisha kumtakia siku njema ya wapendanao.

Valentine! Mwongozo wa Mapenzi siku ya Wapendanao Pamoja na PODCAST maalum

dennis.and.mariga

Awali Dennis kupitia mtandao wake wa kijamii alimkaribisha Jowie katika dunia iliyo na uhuru huku ikiwalazimu KOT kutoa hisia mbalimbali kuhusu uhusiano kati ya Jacque Maribe, Dennis Itumbi na Joseph Irungu.

“Mr Jowie Irungu karibu katika dunia iliyo na uhuru, najua jinsi kuwa kizuizini inauma na vile huna huru kwa muda

Kwanza Jacque Maribe ni rafiki yangu sana familia yake ni marafiki zangu na watazidi kuwa marafiki zangu, na marafiki wa Jacque pia ni marafiki zangu.” Alizungumza Itumbi.

Kuhusiana na kesi iliyo katika mahakama, Itumbi alisema kuwa si haki kwa Jowie kukaa wakati huo wote kizuizini.

“Tuzidi kuwaombea Jowie, Maribe na familia ya Monicah ili wapate haki, aliyehusika katika mauaji hayo akamatwe na polisi na ambaye hakuhusika aachiliwe huru. Tunataka haki kwa wote.” Alisema Itumbi.

Nyimbo 10 za kuzuzua hisia ukisherehekea valentines

Akizungumzia siku ya wapendanao alisema hana mpenzi wa siku hiyo huku akimwambia Jowie kama hana pesa ya kutuma maua amuitishe atampa atumie kipenzi chake maua.

“Kwa hakika ameachiliwa wakati mzuri wa siku ya wapendanao, na namtakia siku ya wapendanao njema, na kama hana pesa ya kutosha ya kumtumia mpenzi wake maua, nitampa maua ampelekee mpenzi wake.” Dennis Itumbi Alisema.

Give hugs and Kisses!,offa za siku ya wapendanao hapa

Aliongeza na kusema anatumai atapata bahati siku hii ya leo na kusema, atamsaidia pahali popote anahitaji msaada wake kwa chochote kile.

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments