nameless

Nameless afichua jinsi yeye na Wahu hutatua tofauti zao

Msanii wa kizazi kipya Nameless na ambaye ni mumewe mwanamziki mwenza, Wahu amefunguka sana kuhusu ndoa yake na sanaa ya muziki katika kipindi kinachoruka kupitia redio jambo Bustani la Massawe .

Msanii huyu amedokeza waziwazi kwamba ndoa yake na Wahu mbeleni ilikuwa inakumbwa na matatizo na kupelekea wao kukosana habari zinaenea katika magazeti na mitandao ya kijamii.

nameless 1

Ili kutatua matatizo yanatokana na tofauti zao huwa wanafanya mipango karibu mara moja kwa mwaka na kutembelea washauri wa ndoa “Huwa tunatembelea washauri wa ndoa tuseme mara moja kwa mwaka wakati kunapotokea matatizo. Huwa tunashirikisha third party na mtu neutral ili tupate mawaidha ya kuishi vyema,”amesema Nameless.

Amezungumzia kisa na ambapo mpenzi wake alishika ujauzito ghafla walipofunga pingu za ndoa. 

Ili waweze kuishi bila kukosana mara kwa mara mkali huyu amesema iliwabidi wakatenganishe familia na sanaa inayowaletea umaarufu ya muziki.

Changamoto ilikua ni kuelewa tofauti zetu. Shuleni haufunzwi kuishi na watu sisi ni watu wakubwa na kwa hiyo presha ipo.”

Nameless pia amewapa changamoto wasanii wanaofanya kampeni za cheza muziki wa Kenya wafanye muziki mzuri.” Nahimiza wasanii wenzangu wafanye content nzuri na waacha kampeni za kulazimisha madeejay na media zetu kucheza muziki wa Kenya.”

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments