massawe jangwani

Nameless ampasha Massawe baada ya kuanguka katika jangwa la Dubai

Msanii na rafikiye Massawe Japanni, David Mathenge, almaarufu Nameless, alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliomkejeli na kumcheka mtangazaji huyo. Kisa na maana? Alianguka akiendesha pikipiki katika jangwa la Dubai.

Kwa mda wa majuma mawili sasa, Massawe amekuwa Dubai kwa likizo pamoja na marafiki zake ambao wamekuwa wakijivinjari kwa njia tofauti.

“Madereva wa Uturuki ndio wasiojali zaidi duniani,” Massawe afichua

Marafiki hao ambao wamekuwa wakisafiri pamoja na ambao walisafiri na Massawe hadi Mombasa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, tayari wametembelea Dubai Marina Yacht Club eneo la kifahari la burudani, Atlantis, The Palm na maeneo mengine mengi.

Baadhi ya shughuli zingine walizofanya ni kujivinjari ndani ya jahazi (yatch) shughuli ambayo kila mmoja aliyesafiri hadi Dubai huhakikisha kuwa ameikamilisha.

massawe jangwani

Baada ya kuburudika, Massawe na marafiki wake kisha walienda hadi kwenye jangwa la Dubai ambalo ni kivutio kikuu kwa watalii duniani kote. Humo walipata fursa ya kuendesha pikipiki spesheli iitwayo, quad bike.

PICHA: Baada ya kutesa Mombasa Massawe asafiri hadi Dubai

Katika harakati hiyo, Massawe ambaye alikuwa anarekodiwa akiendesha pikipiki ile, alijapata taabani baada ya kuigonga pikipiki iliyokuwa imeegeshwa na kuanguka mchangani tifu!

Massawe alichapisha video ile kwenye mtandao wake wa Instagram na wengi akiwemo, Nameless walimcheka kwa ajili ya jinsi alivyoanguka.

Nameless aliandika: Action movies achia waindi wewe… 😜😜

Mcheshi Njugush naye alisema: 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Mwanahabari Lulu Hassan ndio pekee aliyemjali Massawe huku akisema: We mamaaaaaaaa my heart almost skipped a beat…hope hukuumia lakini.

Jasper Murume aliandika: Vile madem ukufallia ukiwa na subaru.

Tazama video hii ya kuchekesha.

PICHA: Tazama jinsi Massawe Japanni alivyosherehekea siku ya kuzaliwa

Photo Credits: Massawe

Read More:

Comments

comments