Nameless amtakia mwanawe Tumiso furaha siku ya Kuzaliwa

Mwanawe Nameless na Wahu, Tumiso amevunja ungo na sasa wazazi wake wamejawa na furaha kutokana na jambo hilo. Wawili hao walishindwa kufungia furaha yao walipoleka mtandaoni kumtakia mwanao siku njema ya kuzaliwa.

"Amekuwa akizungumzia kuhusu kufikisha umri wa miaka kumi na mitatu tangia mwaka uliopita,' Wahu alisema.

Babaye Tumiso, Nameless alimtakia mwanawe siku njema kwa kumwandikia ujumbe mdogo,"Yooo.... teenager in the house! So proud of the lady you are becoming. Happy 13th birthday Tumiso."

Mamaye mzazi kwa upande mwingine hakuachwa nyuma,"Happy Happy birthday to this angel of mine who gave me the title "mum"!! Ever since you came my way, My whole life has changed... And I do not regret. This beautiful feeling of sweet love."