'Namjua atakayeichukua nafasi yangu,' Kocha wa Liverpool afichua

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa mrithi wake klabuni hapo atakuwa kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard ama kocha wa zamani wa klabu hiyo forme Kenny Dalglish.

Kwingineko, makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi baada ya kukubali kichapo cha kushtukiza dhidi ya Newcastle. Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Solskjaer. (Sun)

Hayo yakijiri, Kocha wa Arsenal Unai Emery anapiga hesabu za kumnunua beki wa Wolves Willy Boly. Wolves wanaweza kutaka dau la pauni milioni 20, wao walimnunua nyota huyo raia wa Ivory Coast kwa pauni milioni 10. (Sun).

Kwingineko, Real Madrid wapo tayari kuchuana na Juventus ikatika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante. Vigogo hao wa La Liga wanaweza kulipa dau la uasajili la kufikia pauni milioni 70 ili kumnasa Mfaransa huyo. (Sport, via Mail)

Tukisalia Chelsea, Winga wa Chelsea Christian Pulisic,21, anaripotiwa kutaka kuomba kutolewa kwa mkopo kama hatapata muda mwingi zaidi wa kucheza klabuni hapo. (Sun)