Nana Owiti asimulia ndoa yake na rapa King Kaka, ataja kukosana

owiti_nana_and_hubby__1569823937_31650
owiti_nana_and_hubby__1569823937_31650
Mkewe King Kaka Nana Owiti amefunguka na kusema kuwa uhusiano wake na rapa huyu sio kamilifu.

Kama ndoa za kawaida wawili hawa ukumbwa na songombingo za mahusiano.

Akizungumiza uhusiano wao, Nana ameripoti kuwa mara kwa mara huwa wanakosana na kutokubaliana.

Soma hadithi nyingine:

Nana amesema kuwa King Kaka hajawahi kumnyoshea kidole ata siku.

https://www.instagram.com/p/B23f1m4nlT_/

" Tuna mchanganyiko wa mapenzi na vita. Huwa tunacheka, tunalia, tunapigana na cha msingi zaidi huwa tunakaa na kusuluhisha mambo..."

"Sijawahi ata siku mkaripia kwa sauti mme wangu.."

"Yeye pia hajawahi nikaripia wa sauti wala kuninyoshea kidole au kunipiga..." Aliandika Nana.

https://www.instagram.com/p/B268OcPHAWD/

Wanandoa hawa wamejaliwa watoto wawili.

Soma hadithi nyingine:

Nana anamtaja King Kaka kama baba wa kuigwa na kupigiwa mfano.