Kati ya Bahati na Willy Paul nani mkali wa mavazi?

Sanaa ya nyimbo za injili nchini inakuwa  na inaendelea kukuwa kila siku ambapo wasani chipukizi wanainukia kutoka viwango tofauti hadi vingine kama njia ya kudhiirisha ubabe wao kwa waliokolea kwa katika sekta hiyo.

Kupitia kwa nyimbi,mavazi nywele na mambo mengi,  wasanii hawa wanajulikana sana kwa miondoko yao ya mavazi ambayo huacha wengi wakitokwa na mate.

Wakiwa na panda shuka zao maishani,wawili hao hawajawaangusha mashibiki wao kwa mavazi na hata kwa kushindana nani kuwa ni nani atatoa mziki mtamu na nyingi.

Willy Paul anajulikana  saana kwa uimbaji wake na hata  kama mwandishi wa nyimbo.

Ameimba nyimbo ambazo zimechezwa sana na watu wengi kama vile Sitolia, Kitanzi, Fanya na nyimbo zingine, Aidha alizawadiwa mwaka wa 2013 kwa kuwa msanii bora wa kiume wa mwaka.

Ikija katika maridadi ya mavazi mwanamziki huyo anajua kujikakamua na pia kuwashangaza wengi jinsi anavyo vaa kwa hafla tofauti.

Bahati pia ni mwanamziki wa nyimbo za injili ambaye  ametoa nyimbo ambazo zimependwa na wengi na pia zimechezwa sana.

Mwanamziki huyo alijulikana mwaka wa,2012, alipotoa wimbo wake wa 'mama' Bahati pia kwa muda hajabaki nyumba ikikuja kwa upande wa mavazi.

Kwa hafla tofauti huwa anajitoa awezavyo na pia kuwaacha mashabiki wake wamebutwaa kwa sababu ya alivyo vaa.