Naogopa-VIDEO-STUDIO-640x300

Naogopa ni wimbo wangu,Nitamfunga jela, Rayvanny afoka

Staa wa Bongo Rayvanny amefungukia Bongo 5 kuhusu skendo ya msanii mchanga kutoka mkoa wa Iringa anayelalama kuwa ameiba wimbo wake wa Naogopa.

“Nafikiri serikali itusaidie kwa hili kwa sababu imekuwa too much. Watu wamekuwa sana wakitaka tension kupitia watu. Ujue mimi nime-hustle sio chini ya miaka sita saba huko. Nimeteseka saana kupata nafasi nikonayo ka sasa…” Amesema Rayvanny.

Dakika 5 tu niage dunia, Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki afunguka

Rayvanny alishangaa kuona msanii ana wimbo kama wake, neno baada ya neno.

“Katika niymbo zote nimeimba yaani nikuje niibe Naogopa. Noo siwezi fanya huo upumbavu…” Alifoka Rayvanny.

(+Picha) Umaarufu wa watoto wa Diamond Platnumz, idadi ya wafuasi Insta

Rayvanny ameshikilia kuwa Naogopa ni wimbo wake.

“Naogopa ni wimbo wangu. Ni utunzi wangu. Kila kitu nimeiandika mwenyewe. Nafikiria huyo dogo popote alipo anajua….” Aliendelea kuongea.

Staa huyu ametishia kumshtaki kijana huyo.

Image result for naogopa by rayvanny

“Saa hizi tunapoongea na wewe naweza kwenda kumshtaki. Naweza kwenda kumshtaki. Ila hana hela ya kunilipa. Ndugu zake watapata tabu. Ifike time wawe na Respect…” Rayvanny.

Acapella ya Naogopa inafanya freshi na inashika nafasi nzuri katika mtandao wa YouTube.

“Sio wizi, ni malipo ya Twa twa twa,” ajitetea Ruth Khaecha mbele ya korti

“Mimi siwezi kuiba wimbo maana ubongo wangu bado mbichi sana, siwezi kukaa eti nisikilize wimbo wa dogo kama huyo ni copy verse ya kwanza Verse ya pili halafu niirekodi nipost kitu kisichowezekana “ Alisema Rayvanny.

Rayvanny anasema kuwa wimbo huu ulivuja kitambo.

Image result for naogopa by rayvanny

“Wimbo ni wangu mimi. Yule dogo kauchukua na kuimba ule wimbo vilevile. Wimbo wangu ulivujaga kitambo. Ni nyimbo zangu nyingi hazikutokaga. Watu wahustle wapambane kwa bidii.” Rayvanny.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments