'Naomba msamaha,' Raila Junior aomba msamaha baada ya kusutu chama cha ODM

Raila
Raila
Baada ya Raila Odinga Junior, mwanawe kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, kusuta vikali chama hicho kwa kupoteza mwelekeo, hatimaye ameomba msamaha kama taarifa yake haikueleweka alivyokuwa anataka huku akisema maoni yake hayakuwa yanalenga kiongozi yeyote.

Katika taarifa, Junior alidai kuwa chama hicho kimeanza kujihusisha na siasa mbaya na kusahau wajibu wake mkuu kuhusu kuhakikisha kuna huduma bora, demokrasia na kulinda haki za Wakenya.

"Sisi kama ODM tunatakiwa kujirudia, wajibu wetu sio kupanda ndege na slay queens huku tukiwatusi wanasiasa mahasidi, tuna ajenda ya maendeleo ambayo imechapishwa kwenye manifesto yetu, tuzingatie utoaji wa huduma, demokrasia na kulinda haki za Wakenya." Aliandika Junior.

NI ujumbe ambao uliibua mdahalo kwenye mitandao ya kijamii na kisha Raila Junior kuomba msamaha na kusema kuwa,

"Kwa kufafanua kama mwanachama wa kawaida wa chama cha ODM maoni yanguu ni ya kwangu na wala si ya chama,2.nashukuru kwa ajili ya ODM kwa kufuata demokrasia ambapo maoni tofauti hutolewa 3. Maoni yangu hayakuwa yanalenga kiongozi yeyote naomba msamaha kwa kutoelewana." Aliomba Raila Junior.