'Naomba mume wangu aambukizwe kisonono afariki!' - Cynthia

Je wewe kama mwanaume ukaskia kwamba mkeo hukuombea mabaya ili uage dunia utafanya nini? Utamuombea abadilike au utamtema kama viazi moto?

Katika kipindi cha Bustani la Massawe, mwanadada mmoja aliwaacha wengi vinywa wazi alipopiga simu na kulalamikia tabia za mumewe.

Kulingana na mwanadada yule kwa jina Cynthia, alisimulia jinsi mumewe amekuwa fisi mla wanawake njia ya ndoa, jambo ambalo linamkera sana moyoni mwake.

Alidai kuwa mumewe ana mipango ya kando wengi na huwabadilisha kila siku kama nguo.

Cha kushangaza ni kuwa Cynthia ambaye amekuwa kwa ndoa ya miaka minane na jamaa huyu, humuombea usiku na mchana apate maambukizi ya kisonono.

Anadai ombi lake ni kuwa akipata kisonono atakosa zile nguvu za kutongoza wanawake na mwishowe aage dunia.

Ila alichosahau Cynthia ni kuwa kisonono kina dawa na waweza kupona ukinywa dawa vilivyo.

Hata hivyo soma usimulizi wake;

Wangu amefika mwisho yaani naombanga mungu kila siku apate kisonono agonjeke ashindwe kutongoza wanawake. Amenifika mwisho aki ya mungu huyu mwanaume ni malaya anatembea kwa wanawake kila siku ananibadilisha kama nguo.

Je si akipata kisonono atakuambukiza?

Hapana hawezi juu mimi hatuwezi shiriki na yeye ndoa, tumeishi naye miaka minane na baada ya kujua ana hao wasichana nimekaa karibu miezi sita hivi hatushirikiana.

Niko tu sawa lakini mimi huomba usiku na mchana apate kisonono agonjeke akufe!