Lakini sasa fahamu kwamba kuna wanaume ambao pia hufanya ukahaba kwa kuuza miili yao na kulipwa! Sikuamini kuna wanaume wanaofanya kazi kama hiyo hadi pale Justus Moto alipokubali kunisimulia maisha yake kama kahaba wa kiume na jinsi anavyoishi maisha ya starehe kwa hisani ya wanawake kadhaa ambao ni wateja wake na wanaofahamu jinsi anavyowahudumia kwa kuwapa kila raha wanazotaka katika nyumba zao .
Justus anasema alijipata katika kazi hiyo wakati alipokuwa Model wa kiume na baada ya msururu wa kazi za maonyesho akivalia nguo za lebo moja ya Afrika Kusini. Mwanzoni aliwavutia wanawake wa rika lake ambao wengi walivutiwa na kuunga kwa mwili wake na mara nyingi uhusiano kati yake na wasichana hao uliishia kwa One Night stands ngono za usiku mmoja bila makubaliano ya uhusiano wa kudumu. Muda sio mrefu, Justus aligundua kwamba kuna wenzake katika kampuni yake ya modeling ambao walikuwa wakiishi maisha ya gharama ya juu, na alishangaa waliwezaje kugharamia mtindo wao wa maisha .
Akiendelea kujikuna kichwa kugundua siri, alinong’onezewa kuhusu ‘biashara’ ya pembeni iliyokuwa ikinoga kwa Models wa kampuni ile ya kuwapa huduma za ngono wanawake ambao hawakuwa na waume, na wa umri wa juu na waliokuwa na pesa kama njugu! Justus alijua kwamba uwanja huo mpya ulioonekana wa kuvutia utamletea matatizo baadaye lakini pia alivutiwa sana na pesa na mtindo wa maisha ya kifahari ambao ulikuwa umemngoja endapo angekubali kujiingiza katika biashara hiyo. Muda sio mrefu, Justus alikuwa keshafanya uamuzi wake na wateja walikuwa wengi na walimtaka kila wakati. Mwanzo, mteja alimfahamisha siku ambayo alimhitaji na kupitia kundi la whatsapp, waliunda ratiba. Akina mama hao wengi wao wakiwa wafanyikazi wazito katika mashirika makuu ya umma na kibinafsi na wafanyibiashara tajika. Biashara hii ya mahakaba wa kiume ipo hapa Kenya na inaendeshwa kwa usiri mkubwa .
‘ Unashangaa kuwaona baadhi ya hata wasanii wakiishi maisha mazuri, kuna kazi inayoendelea chini ya maji na ina pesa’ anafichua Justus
Kuhusu malipo, Justus anasitasita kabla ya kusema kiasi cha fedha ambazo yeye hutoza kwa huduma zake . Malipo , anasema yanategemewa na muda ambao mteja atataka awe naye. Usiku mzima kwa mfano ni shilingi elfu 25 kwa mteja ambaye uhudumiwa angalau mara nne kwa mwezi . Wateja wapya hutozwa kiasi cha juu kwa sababu ya kuweza kuwachuja wale ambao labda wanaleta mchezo katika ratiba zao na kusalia tu na wateja ambao watakuwa wa kila mara .
‘ Kupitia kazi hii ya kisiri ,nimweza kujenga nyumba na hata kuwekeza hapa Nairobi na mashambani’ Justus anasema .
Justus anasema wengi wa wateja wake ni wanawake wa umri wa juu ambao wametelekezwa na waume zao au ni wajane. Anasema anapenda kuwahudumia wanawake wa umri wa juu kwa sababu hawasumbui na wao hujua wanachotaka pindi tu wanapoagiza kupata huduma zake .
‘ Sisi huwaita mashosho – ni wakarimu and mostly hamsumbuani kuhusu malipo.wanajua nipo kazi na mimi huwasikiza hata wakati ninapoendelea kuwapa starehe zao’ anasema Justus
Justus anasema jamii inafaa kujali maslahi ya wanawake wa umri wa juu kuanzia maiaka 40 ambao hawana wapenzi na wanaohitaji ngono. Anasema ni ubinafsi kwa watu wa umri wa chini kuwasulubisha wanawake hao ama kufikiria kwamba nao pia hawahitaji joto katika vitanda vyao . Licha ya usiri mkubwa unaohusishwa na biashara yao, Justus anasema ameyaona makubwa na baadhi ya siri za wateja wake humfanya kububujikwa machozi .
‘ Kuna mteja wangu ambaye mume alimuacha kwa sababu ni mnene kupindukia, kabla ya kujulishwa kuhusu huduma zangu, alikuwa ameishi miaka mitano bila kushiriki ngono’ anasema Justus
Justus anaongeza kusema ;
‘ Wakati mwingine, hata kama wengine watasema ni utani, mimi hujihisi kwamba natekeleza wajibu muhimu kwa jamii, wanawake wanaotumia huduma zangu kupata ngono huridhishwa na kuwezeshwa kuhisi vizuri kama tu watu wengine’ anatamatisha Justus .