Mwanawe wa Diamond na Tanasha ashereheka siku 40 za kuzaliwa

Diamond Platnumz na Tanasha Donna walifichua jina la mtoto wao wa kwanza na ni wazi kuwa familia hii inataka tu jina lao la familia libaki kwani Diamond na  Tanasha walimpa mtoto wao jina la babake ambalo pia ni jina la Diamond mwenyewe.

Naseeb Junior ndilo jina  la mtoto huyo na ana mashabiki 68,000 katika mtandao wa kijamii wa Instagram licha ya umri wake mchanga.

Jana Naseeb alisherehekea siku ya arubaini tangu kuzaliwa kwake, sherehe ambayo ni muhimu sana kwa waislamu.

Aqiqah ambayo ndiyo sherehe yenyewe husherehekewa kwa kuchinjwa kwa mnyama kuashiria kuzaliwa kwa mtoto na desturi ya waislamu, nyama hii hugawiwa maskini na mayatima.

Diamond kwa sasa yuko ziara ya kibiasha.

Kupitia mtandao wa kijamii,mamake Naseeb aliandika,

'Thank you, God, I’m blessed to be here, with that said…. I’ll be right back instafam. 👼🏽💞'

Licha ya hayo, kilichonifurahisha na sherehe hii ama desturi hii ni kuwa mamake mtoto hafai kutoka nyumbani kabala ya mtoto wake kupitisha siku 40 lakini Tanasha alianguka mtihani huu.

Tanasha alitoka nyumbani baada ya siku 20 kujifungua jambo ambalo ni kinyume na dini ya kiislamu.

Vilevile, binti huyu anafaa kukaa na mama yake au mama mkwe katika siku hizo 40 .