'Nashuku mke wangu aliua mtoto wetu,' Jamaa asimulia

Jamaa kwa jina William alipiga simu katika kipindi cha Bustani la Massawe akisimulia kuwa aliwachwa bila majibu baada ya mwanawe kufariki.

Cha kushangaza ni kuwa mwanawe aliondoka na mkewe akiwa buheri wa afya kabla ya kupigiwa simu wiki mbili baadaye akipashwa habari kuwa amefariki.

Akijaribu kutafuta majibu kutoka kwa mkewe, mkewe alikuwa analihepa swala hilo. Hilo lilipelekea wawili hao kupigana na baada ya matanga ya mwanao kuisha, mkewe alikimbia kwao nyumbani.

Alipojaribu kuwazungumzia wazazi wake walikataa mkewe arudi kwake na isitoshe, kufikia sahii bado hajibu simu zake na hilo lamfanya kushuku kuwa huenda yeye ndiye aliyemuua mtoto wao.

Soma usimulizi ufuatao.

Nilikuwa na mrembo na tukapigana akaenda. Tulipigana kwa vile mtoto aliaga dunia baada yake kuniwacha Nairobi mtoto akiwa mzima.

Baada ya wiki mbili nilipigiwa simu nikiambiwa kuwa mtoto amefariki, kumuuliza sababu ya kifo chake hakuniambia. Hapo tukaanza kupigana na matanga yalipokamilika akaenda kwao, kwenda kwao kuzungumza na wazazi, wakakataa arudi.

Kufikia sahii nampigia simu hawezi kuzungumza kumbe alikataa kabisa. Nilikuwa namshuku kuwa yeye ndiye alimuua mtoto wetu.

&t=7s