Akothee atishia kumnyoa mpenzi wa binti yake, Rue

Esther Akoth almaarufu Akothee hajafurahishwa na mtindo wa nywele wa mmoja wa wacheshi wa Kenya ambaye ana uhusiano na bintiye Rue kwa muda sasa.

Akothee ametishia kumnyoa 'mkwe wake' na kumtaka bintiye Rue kufikisha ujumbe.

Lakini ni nini kilicho sababisha rais wa kinamama kusema maneno haya? Hii ni baada ya Akothee kumuuliza mwanawe Rue baby vile mpenziwe ambaye ni 'comedian' alivyokuwa anaendelea.

Akothee alisema kuwa anataka kunyoa mcheshi huyo nywele zake.

Katika ukurasa wake wa Instagram Akothee aliweka video akimshauri Rue kwamba kama anataka mpenzi au mchumba anapaswa kutafuta mwanamume ambaye hana nywele kama za msanii huyo kwa sababu watu wenye mitindo ya nywele kama hiyo ni wasumbufu sana.

"Mpenzi wako anaendelea aje? kwanini unakasirika na kupatwa na hisia hizo ama junadhani sijui," Aliuliza Akothee.

Katika matamshi yake Akothee alimwambia mwanawe kuwa kama anataka kuwa katika uhusiano lazima mpenzi wake anyoe.

La sivyo atakuwa anaitisha pesa za kusongwa mara mbili .

if you think of dating a man let him shave his hair please ,you will not ask for double saloon money 🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️ men with this kind of hair is troubles 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️.

Msanii huyo hata hivyo alijibu ujumbe huo wa kunyolewa na kumwambia Akothee kwamba ni yeye ataita polisi.
"Leo ni mimi nitawaita polisi mayooooooo," Tricky Aliandika.
Wawili hao wamekuwa katika uhusiano kwa muda sasa na dada yake Rue Vesha Shaillan amedai kwamba wamekuwa na ushusiano kwa muda.
Lakini wawili hao ni marafiki ama ni wapenzi hii ni kwa sababu msanii mpenzi wa Rue alisema kuwa amemchumbia mwanamke mmoja mrembo anaye fahamika kama Renee ambaye amekuwa akionekana katika filamu zake kwa muda.