'Nauza account' Aina 5 ya watu utakaopata kwa Instagram ya maceleb

Kwa sababu nisizoweza kupeana kwani pia mimi inanishinda, ni kuwa mara kwa mara mimi hujipata nikikimbia katika akaunti za ma celeb haswa mahala ambapo mashabiki hutoa maoni yao.

Sababu moja yaweza kuwa mimi huelekea humo kujiburudisha na maoni ya mashabiki, ya pili huwa kutafuta celebs ambao wanawamezea wenzao mate na pia kuona kama kuna matukio yoyote humo, baina ya ma celebs na wafuasi wao.

Kwa hivyo katika pilkapilka zangu, niliweza kutathmini mambo kadhaa yasiyo ya kawaida katika mitandao hiyo ya ma celebs.

Leo nimeamua kukupa aina tano ya watu ambao huyawahi wakosa pale kwa 'comment section' za ma celeb wote, iwe Kenya au ulaya, kwani binadamu ni walewale.

Niliweza kufanya uchunguzi wangu katika mitandao ya Instagram ya Diamond Platnumz na Akothee, na kusema ukweli, wakenya na watanzania wana tabia kama za pacha wawili.

Hawa ndio aina 5 ya watu ambao hutawahi kosa,

  1. Wanaopiga biashara

Hawa ni wafuasi ambao watangoja celeb achapishe chochote, kisha wangoje kwa mda flani na watu wakiongezeka mle ndani hapo ndipo wataingia na kuanza kuuza bidhaa vyao.

Baadhi ya vitu wanavyouza ni akaunti za Instagram, simu na hata pia kadi za simu.

Ifuatayo ni mifano kadhaa;

Mr Bundle: Nakuunga na kifurushi bei ndogo sana, kuanzia GB 60 miezi 3 hadi GB 320

Followers Tz: Wanaohitaji kuongeza 10k followers wanich in box

Nauza account za insta: Anae hitaji account kuanzia ukubwa huu muitaji DM me halaka sana 10.2k 13.9k 16k 17.2k njoo dm tufanye biashara.

  1. Wanao omba kupata wafuasi wengi almaarufu 'Follow back battalion'

Wafuasi hawa huwa macho wakingoja celeb yeyote achapishe lolote kabla ya kukimbia mle nda kuomba wafuasi wengine wampe 'follow' 

Mfano,

I am Akothee's fan please follow me

  1. Waliojawa na chuki

Kama tujuavyo sio kila mtu atapenda au kufurahishwa na kile unachofanya hata uwe mfano mwema aje.

Wafuasi kama hawa huwa tu wamejawa na chuki na hasira zao na hutafuta mahala ambapo wataangusha hasira zao. Wengine wao hufanyi hili ili tu kupata 'likes'

Tazama mifano kadhaa;

Wacha utoto na wewe ni mtu mzima 

Hiyo trouser yako ni tent sanaa

  1. Wanaotafuta kazi

Dunia ina mambo na huu wengine wakisherehekea mali nyingi, wengine wanatafuta kila namna ya kutolala njaa na kulisha familia zao.

Wengi wa wakenya hawana kazi na hutafuta kila namna ya kupata ajira, moja yapo ikiwa kuwaomba celebs hao kazi.

Please madam I need a job pliz help me any kind of job I will do

  1. Mashabiki wa ukweli

Kundi hili nalo ni la wafuasi wa ukweli ambao wanampenda celeb yule kwa kile anachofanya na jinsi anavyojiwakilisha kwa jamii.

Ukisoma maoni yao huwa ya kuwapa maceleb wao nguvu na pia kuwapongeza kwa kile wanachofanya.

Hawa ni baadhi ya wafuasi niliopatana nao kwa akaunti ya Instagram ya Akothee.

Wow I really like your energy you are my role midel. Love you

You are a blessing to our country

Akothee for women rep 2022

Mom always smart

Keep being blessed queen