NCIC imewashauri wakenya kudumisha utulivu na uvumilivu wakati mashirikahusika ya serikali yanapochunguza suala hilo . Sudi siku ya jumatatu alijitokeza akwa maneno makali alipokuwa akimtetea mbunge wa Emurua Dikiir Johanna Ng'eno aliyekamatwa pia kwa kumzungumzia raisUhuru kenyatta na na mamake rais Mama Ngina Kenyatta .
Polisi huko Transmara Mashariki walimkamata Ng'eno kwa matamshi yake ya uchochezi dhidi ya rais Uhuru kenyatta nafamiliayake .
Akikubaliana na Nge'no Sudi alilalamika kuhusu hatua ya rais kenyatta kumtenga naibu wake licha ya kumsaidia kushinda uchaguzi mara mbili .
“ Nataka kumuambia rais kwamba hatuna deni lake ,tulikupigia kura mara tatu -mwaka wa 2013 na 2017 mara mbili ..nchi hii ni yetu sote' Sudi aliyekuwa nahamaki amesema
aliongeza kusema kwamba rais kenyatta amemsaliti naibu wake William Ruto na ameonekana kumtenga katika serikalialiosaidia kuunda . Matamshi yake hata hivyo yamekosolewa hata na Naibu wa rais mwenyewe .Ruto amesema viongoziwanafaa kuishemu afisi ya rais na rasi Uhuru kenyatta