Ndege ya pili iliyowabeba wakenya kutoka Uingereza i njiani yaja - Esipisu

kq-e1589547067738
kq-e1589547067738
Ndege ya pili ambayo imewabeba wakenya kutoka Uingereza kufuatia mlipuko wa virusi vya corona ipo njiani. Kulingana na balozi wa Kenya nchini humo, Manoah Esipisu, ndege hiyo ya shirika la Kenya Airways ilitoka katika mji wa Haethrow mida ya 3 jioni jana.

Jumanne, ubalozi huo ulikuwa umetangaza kuwa ndege ilikuwepo ya kuwabeba wale wanaotaka kurejea nchini japo kwa masharti.

Wakenyua ambao walikuwa wametangaza wanataka kurejea nchini walilazimika kulipa kati ya shilingi 101,000 kwa kila tiketi na katika kitengo kingine ama economy class walizamika kulipa shilingi 290,000 kwa kila tiketi.

Ikielezea tofauti kubwa za tiketi hiyo, KQ ilisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inabeba mizigo kutoka na kupeleka mizigo katika taifa hilo.

Baada tu ya kutia guu nchini, wakenya hao watawekwa chini ya karantini kwa siku 14 -28 kwa gharama yao wenyewe.

Wakenya wote waliokuwa wamekwama Uchina na India walirudishwa nchini.