Ndio hawa:Orodha ya wanahabari waliopatikana na virusi vya corona

1595916424820(1)
1595916424820(1)
Virusi vya corona viligunduliwa nchini China mwaka jana Desemba, ni virusi ambavyo vilisambaa sana katika nchi tofauti huku kisa cha kwanza humu nchini kikiripotiwa machi,13 mwaka huu.

Kufikia sasa idadi ya watu waliopatikana na virusi hivyo nchini kenya 14805, huku wengi wakizidi kupona virusi hivyo, Kenya imekuwa ikirekodi visa vipya vya virusi hivyo kila kuchao.

Ni virusi ambavyo vimeathiri sekta mbalimbali hasa sekta ya uhanahabari huku wanahabari tofauti wakiambukizwa virusi vya corona.

Hawa hapa baadhi ya wanahabari ambao wameambukizwa na virusi hivyo kufikia sasa;

1.Jeff Koinange

Mwanahabari wa runinga ya Citizen na mtangazaji wa redio ya Hot96 alipatikana na virusi hivyo siku ya jumatatu,20, Julai.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii Jeff alitangaza habari hizo, huku akisema hakuwa na dalili zozote za maradhi hayo.

2.Bonnie Musambi

Mtangazaji wa KBC Musambi kupitiaa kwenye mitandao ya kijamii aliposti picha ya matokeo yake huku akiwa ameambukiza virusi hivyo.

3.Stephen Letoo

Mwanahabari huyo wa runinga ya Citizen anafahamika sana kwa bidii na ustadi wa kazi yake ya uhanahabari, mnamo tarehe,17,Julai alithibitishwa kuwa na virusi hivi huku akijitenga ili hasiwaambukize wenzake.

4.Ian Wafula

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii alitangaza matokeo yake ya vipimo vya virusi na kusema kuwa anaendelea salama licha ya kupatikana na virusi hivyo.

Nimesema haya mitandaoni ili watu wajue kuwa ugonjwa huu upo, na hata kukomesha unyanyapaa na ili tuwe salama mimi na dada yangu tutajitenga nyumbani licha ya kupata virusi hivi, yuko sawa lakini hajaonyesha dalili zozote za corona."Baadhi ya ujumbe wake ulisoma.

5.Miss Katiwa

Mtangazaji wa runinga ya NTV alifichua haya jumapili iliyopita na kudai kuwa ana virusi hivyo.

Ni jukumu letu kama wananchi kujikinga na virusi hivi, kwa maana hamna mtu yeyote angetaka kumpoteza jamaa au rafiki yake kwa ajili ya virusi hvio. tunawatakia afueni ya haraka.