Ndoto Butu? Msanii Bahati asema siku moja atakuwa rais wa Kenya

Mwanamuziki Bahati huenda ana amaazimio mazito kuliko uzani wake .

Baada ya kuwa katika ndimi za wengi wa kufaniwa mzaha mitandaoni hivi karibuni kw ajili ya wimbo wa Kaligraph kwa jina ‘ hao’ bahati sasa anasema siku moja atakuwa rais wa Jamhuri ya Kenya . Katika wimbo wake ,Kaligraph alimpiga Bahati kijembe kwa kumtaja kama  ‘Bahati mtoto wa  Diana ,mstari ambao uliwafanya wengi kumpiga kejeli msanii huyo  aliyetamba kwa wimbo ‘mama’.

Hakusazwa  katika mitandao kwani alianza tena kuchanwachanswa wakati alipotoa video na Diana wakiwadensi huku Bahati akiwa amevalia nguo za mwanamke . Jana msanii huyo aliamua sasa kugonga msumari mwingine katika kidonda cha mashabiki wake katika instagram kwa ujumbe ambao bila shaka ulilenga kuzua majibu ya kila aina .

Alitaka kuheshimiwa na watu katika twitter  na kuahidi kwamba siku moja atakuwa rais wan chi  .Ujumbe wake ulisema hivi ;

 “I will be the President of this Country One Day  So Tell those Keyboard Warriors on Twitter to Come Srowwree and Address Me With Respect!… hio Ndio Kitu Ya Kwanza Nitafunga Nikiapishwa  #MrBahati.”

“Twitter is the First thing I will burn Once I’m Sworn in as the President of Kenya. Aki Simnasumbuaaa #BAHATI,”  Bahati alisema

Kilichofuatia ni  kejeli zaidi huku wengfi wakipuuza uwezo wake  kuongoza hata kanisa lolote