Ndoto za Abunuasi! Gavana Mutua asema atawania kiti cha Urais mwaka 2022

Alfred Mutua, gavana wa Kaunti ya Machakos amewaacha wengi vimywa wazi baada ya kusema kuwa atawania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2022.

Akiwa kwa mazungumzo na Radio Jambo, Mutua amesema wakati umefika wa vijana nchini kuchukua hatua na kuanza kunyakua nafasi za uongozi ambazo zipo.

Amesema kutokana na miradi ambayo ameitekeleza katika kaunti ya Machakos inamfanya yeye kuwa kiongozi shupavu na ambaye anaweza  kuipeleka Kenya katika kiwango kingine.

“There is a difference between leaders and politicians. Healthcare is an important thing for me because now Machakos Level five looks like a private hospital I have hired 800 nurses. AmesemaMutua.

Mutua amesema jitihada za kuafikia malengi hayo yote katika kaunti ya Machakos haikuwa rahisi kwani alikumbana na changamoto si haba ikiwemo mitazamo kinzani kutoka kwa viongozi kwenye kaunti hiyo.

Amesema baadhi ya wanasiasa hao walimpeleka mahakamani kupinga kuteuliwa kwake japo akaibuka mshindi.

When I started doing all these stages to help develop Machakos, some politicians took me to court. By the time the court ruled the case that Mutua was on the right side of the law,  the guy who made Buj Khalifa pulled out on investing here saying they have put their money in other counties. They do not have time to wait. All this is because of the stupidity of politicians. Why should we go overseas to live a good life and we can do it here?” Alfred Mutua alisema.

Akizungumzia hatima yake ya kutaka kuwa rais wa Kenya, Mutua amesema imetimia wakati mimi na wewe kusimama tisti na kuchukua nafasi za uongozi ambazo zipo. Mutua amesema kufikia sasa, viongozi walioko mamlakani wamelitenganisha taifa pakubwa kwa manufaaa yao wenyewe .

It is time for the youth to take over the country and decide who will lead them. Now people are sitting and dividing the country. We have never moved away from pre-independent leadership. The people we have in leadership are of the system of pre-independence. It is our time to decide who is our next leader. Alisimulia Mutua.

Amesisitiza umuhimu wa vijana nchini kushirikiana na ili kufanikisha malengo yao. Amesema kuwa katika taifa la Amerika vijana kati ya miaka 19 na 20 wanaendesha magari yao, hatua ambayo inaweza kufanikishwa nchini iwapo vijana wote watashirikiana na kufanya kazi pamoja.

Amesema swala hilo linaweza kuafikiwa bila ya kuangazia ukabila .

It does matter your tribe gender where you sleep and what you ate, never give up hope because God knows your plan and you can live a good life. Amesema Mutua.