Ndugu waliofungwa kimakosa kwa miaka 24 walipwa dola milioni 3.8

_112969183_eric-simmons
_112969183_eric-simmons

Ndugu wawili wa Baltimore ambao wametumikia kifungo cha miaka 24 gerezani kwa mauaji ambayo hawakuyafanya ,kila mmoja amepokea dola milioni 1.9(£1.5m) kama fidia kutoka serikalini.

Eric Simmons na Kenneth "JR" McPherson waliachiwa huru mwezi Mei 2019 baada ya mwendesha mashtaka kukuta makosa katika uchunguzi uliofanywa.

Matokeo hayo yanajiri baada ya mjadala mkubwa nchini Marekani kuhusu kurekebisha mfumo wa polisi na ule wa haki katika kesi za uhalifu. .

Wanaume wote wawili waliokuwa weusi, na walishutumiwa kuuwa mwaka 1994 .

Walikuwa na miaka ya 20 walipofungwa kwa madai ya kuua mwanaume mwenye umri wa miaka 21- huko mashariki ya Baltimore, Maryland.

Mradi wa wasiokuwa na hatia ambao umekuja na ushahidi mpya kuwa polisi walimshurutisha kijana wa miaka 13-kuwatambua kuwa bwana Simmons na bwana McPherson, na walimtishia kijana huyo mdogo kwa mashtaka ya mauaji iapo angekataa kuwatambua

Shahidi mwingine ambaye alilipwa na polisi kutoa taarifa katika kesi nyingine alidai kuwa aliona tukio la mauaji akiwa katika makazi yake gorofa ya tatu, umbali wa futi 150(45m).

Mwanasheria wa jimbo la Baltimore bwana Marilyn Mosby alisema mwaka jana wakati wanaachiwa kuwa bwana McPherson alikuwa karibu ya eneo wakati wa mauaji hayo na bwana Simmons alikuwa amelala.

Je ndugu hao walipokea vipi uamuzi huo?

Bwana Simmons, 49,alisema licha ya kwamba wanashukuru kupata fedha hizo kutoka bodi ya wafanyakazi wa umma mjini Maryland, lakini hakuna gharama inayoweza kulipa muda waliopoteza gerezani.

"Mama yangu alifariki '09, na sikuweza kumuaga " alisema kwenye Washington Post. "Fedha haziwezi kurejesha muda ambao nilikuwa nimepoteza kwa kufungwa , fedha haziwezi kutatua tatizo hilo.

"Nilikuwa naamka kila siku najiuliza kama ni kweli au naota" alisema, alikumbuka wakati ambao alikuwa akiamka gerezani na kuhisi kuwa yuko nyumbani.

''Rufaa yao iliokataliwa 2010 nusra imshinikize ajitoe uhai'', alisema.

'Iwapo ingekuwa mimi pekee, nisingetka kuamka baada ya hapoNi Mungu tu ndio aliupa pumzi mwili wangu."

Kwa mujibu wa mradi wa ' Innocence 'kulikuwa na watu wengine 30 wenye kesi kama yao walioachiliwa.

Bwana Simmons na McPherson ni wa tisa na kumi kupata fidia hizo kwa kuhukumiwa kimakosa.