Ndugu yangu bado angependa kuondoka Man United - Pogba

mathias.pogba
mathias.pogba
Ndungu ya Paul Pogba, Mathias anasema kuwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa wa miaka 26, bado anataka kuondoka Manchester United na kujiunga na Real Madrid. (El Chiringuito via Daily Mail).

Jadon Sancho anajiandaa kuhama Borussia Dortmund na tayari klabu hiyo ya Ujerumani imeanza kumsaka atakaechukua nafasi ya mshambuliaji huyo wa miaka 19 wa England. (Mail)

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, huuenda akaondoka klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun).

Monaco wanamtaka mshambuliaji wa Uingereza Daniel Sturridge, 29, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Liverpool. (L'Equipe in French)

Kiungo wa kati Mswizi Xherdan Shaqiri, 27, amesema anatafakari hatma yake ya baadae Liverpool ikiwa hatapewa nafasi ya kutosha ya kucheza. (Langenthaler Tagblatt via Daily Star)

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kumkosa mshambuliaji wa England r Harry Kane, 26, huenda kukaiathiri Tottenham ikilinganishwa na kukpoteza huduma ya Christian Eriksen, 27, anasema beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher. (Daily Telegraph)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameelezea furaha yake kuwa James Rodriguez, 28, katika kikosi chake licha ya mchezaji huyo raia wa Colombia hivi karibuni kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Bernabeu. (Corriere dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane
Meneja wa Celtic Neil Lennon anasisitiza kuwa hana mpango wa kumnunua kipa mpya msimu huu. (Daily Record)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 33, ametia saini kandarasi mpya ya miaka mitatu na klabu ya Roma, licha ya tetesi kuibuka huenda akajiunga na mahasimu wa klabu hiyo Inter Milan. (AS Roma)

Winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 21, amabye analengwa na Bayern Munich na Manchester United amethibitishia PSV Eindhoven uaminifu wake kwa klabu hiyo baada ya kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano. (Goal)

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar
Kocha wa Brazil Tite anasema Neymar, 27, anasubiri Paris St-Germain imfanyie uamuzi kuhusu hatma yake ya baadae. (Marca)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa hana uhakika ikiwa usajili wa wachezaji wapya umeimarisha kikosi cha Gunners. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Tottenham Moussa Sissoko anasemekana kuangua kilio baada ya kushindwa katika fainali ya Champions League na Liverpool.(Talksport)

-BBC