Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amechaguliwa bila pingamizi kuwa mwenyekiti wa baraza la magavana . Kupitia mwafaka , magavana wamewaruhusu Oparanya ,Mwangi wa Iria(Murang’a) na Kivutha Kibwana (Makueni) kuhudumu kama mwenyekiti ,naibu mwenyekiti na kiranja wa baraza hilo.
Oparanya ambaye ana uhusiano wa karibu wa kiongozi wa ODM Raila Odinga ametetea kiti hicho kwa muhula wa pili na wa mwisho .Oparanya alichukua wadhfa huo januari mwaka jana kutoka kwa gavana wa Turkana Josephat Nanok ambaye aliongoza baraza hilo kwa miaka miwili .
Washililizi wa nafasi hiyo wameweza kunufaika na ushawishi mkubwa unaombatana na majukumu yao kwani mwenyekiti wa CoG ndiye hutumiwa kama kiunganishi kati ya serikali 47 za kaunti na serikali ya kitaifa . Oparanya ,Nanok na mwenyekiti wa kwanza Isaac Rutto aliyekuwa gavana wa Bomet waliweza kupepezwa katika siasa za kitaifa kutoka na wadhfa huo.