Neymar ajiunga na Christiano Ronaldo na Lionel Messi kwa kutoa msaada kwa waathiriwa wa Corona

79374448_835644786880767_1320663527256314207_n (1)
79374448_835644786880767_1320663527256314207_n (1)
NA NICKSON TOSI

Mshambulizi wa klabu ya PSG Neymar Junior ajiunga na idadi nyingine ya wachezaji maarufu ulimwengunu kwa kutoa mchango mkubwa zaidi kwa serikali ya taifa la Brazil ili kuisaidia kukabiliana na virusi vya Corona.

Kama tu Christiano Ronaldo na Messi walivyofanya katika mataifa yao mtawalia ,Neymar ametoa kima cha euro £775,00 katika taifa lake la Amerika ya kusini ambalo pia limekumbwa na visa vingi vya virusi hivyo.

Baadhi ya wachezaji na klabu kama Barcelona na Athletico Madrid zimekuwa ziktoa michango mbali mbali ili kusaidia serikali za mataifa husika kukabiliana na virusi vya Corona.

Tayari Christiano Ronaldo alitoa mchango wake kwa taifa lake la Ureno sawia na Lionel Messi aliyetoa mchango wake pia kwa taifa la Argentina.