Neymar arejea Ufaransa kujua hatma yake

Mshambulizi wa kiBrazil, Neymar amerejea nchini Ufaransa kwa ajili ya mazungumzo kuhusu hatma yake klabuni hiyo. Neymar, amehusishwa na uhamisho kutoka P.S.G kurejea Barcelona. Neymar alikuwa likizoni baada ya msimu kukamilika.

Hata hivyo, Klabu yake ya paris Saint Germain ilikuwa inamtarajia arejee mazoezini wiki iliyopita ila winga huyo hakurejea kwa madai kuwa likizo yake ilifaa kukamilika wikii hii.

Neymar amewasili nchini Ufaransa hii leo asubuhi kutoka nchini Brazil alikokuwa anatazama mechi za 'Neymar 5 aside'.

Mkurungenzi wa PSG, Leonardo alisema kuwa iwapo kutakuwa na dau la kufurahisha pande zote basi watamkubalia Neymar kurejea Barcelona.

Hiyo jana, Neymar alikitaja kitendo cha kuicharaza PSG mwaka 2017 kama wakati aliowahi kufurahia sana maishani mwake.

"Baada ya kufunga goli la sita, sisi wote tulifurahia sana. Ilikuwa furaha isiyo kifani siku hiyo," Neymar alisema alipoulizwa siku anayoikumbuka na kuipenda kwenye maisha yake ya kisoka.