Ng'ang'a awasuta wanaosambaza video zake, asema wana mapepo

unnamed__2___1569225376_86527
unnamed__2___1569225376_86527
Kasisi mwenye utata sasa anahoji kuwa wanaosambaza video zake katika mitandao ya kijamii ni watu wanaofuatwa na ibilisi.

Kiongozi huyu wa kanisa la Neno Evangelism Centre amegonga vichwa vya habari kwa kuwatusi na kuwapiga makofi wafuasi wake.

Vipande vya video vilisambaa katika mitandao ya kijamii vikimuonyesha James Ng’ang’a akitoa roho chafu katika wafuasi wake kwa kuwapiga.

Soma hadithi nyingine:

Nganga anahoji kuwa video zile ni za maadui wanaolenga kumshusha na kumchafulia jina.

“Huwa nafanya mambo mengi mazuri. Nawapa watu chakula, lakini hao wanakata tu (video)  ile nimeongea vibaya kwa sababu ni watu wana mapepo." Alisema Ng'ang'a

Ng’ang’a alikana taarifa za kutamani kujiua.

"Niliskia taarifa kuwa kuna watu wanasema kwamba waliniona nikiendesha V8 nikiwa na mawazo, ni kama nataka kujia."

Soma hadithi nyingine:

"Hebu tuwe wakweli. Mbona nijiue? Angalia bibi wangu mrembo. Nitamwachia nani nikijiua." alijitetea Ng'ang'a

"Nitaachia nani magari yangu na jumba langu. Labda niwafahamishe majirani zangu ni wazungu. We just say ‘hi’ to each other, hakuna mambo ya kushinda tukibishania mlango.." Aliendelea kujinadi

Aliwaonya mahasidi wake wakome kueneza taarifa za uongo kuhusu ibada zake.