Ng'ang'a hana makosa kuita watu "takataka"- Gilbert Deya

GILBERT-DEYA
GILBERT-DEYA
Baada ya mhubiri wa kanisa la Neno kuwatusi askofu wake na kuwaonya kumpa heshima mpenzi wake. Kasisi mwenye utata Gilbert Deya amefunguka katika kipindi cha Bustani la Massawe katika kituo cha Redio Jambo kuwa haoni makosa ya Ng'ang'a kuwapasha askofu wake.

"Pastor Ng'ang'a ni mtoto wangu wa kiroho. Ni mtumishi wa Mungu. Mungu ya Gilbert ni mungu ya Ng'ang'a na ni mungu ya Elijah. Akisema takataka hiyo si makosa. Ukikuja kunivunja meno nakuvunja wewe kwanza ukiwa kwa dini yake unafaa umtii," asema Deya.

Deya alizungumzia matatizo yaliyoikumba ndoa yake na mpenzi wake ambao kwa sasa wametengana. Hali kadhalika alifunguka kuhusu alivyofungwa jela na baadaye akawa huru.

Tofauti na wengi wanaomkashifu Ng'ang'a akiwemo Askofu wa Kitonga, mhubiri huyu alisema anamuunga mkono na kusema kuwa ni mtoto wake wa Kiroho.

Mengi yanafuata...