Kuna kambi mbili ambazo zinataka kuwa na ushawish na kuamua mwelekeo wa jamii hiyo kisiasa na kumpiga konde Kalonzo anayechukuliwa kama kiongozi wa jamii hiyo kisiasa .Kambi hizo ni moja inayoongozwa na magavana Charity Ngilu, Kivutha Kibwana wa makueni na Alfred Mutua wa Machakos. Kambi nyingine inaongoza na aliyekeuwa seneta wa Machakos Johnstone Muthama ambao inamwunga mkono naibu wa rais William Ruto .
Muthama, kwa upande wake ameliambia gazeti la The Star kwamba Kalonzo na Ngilu wamekuwa na tofauti za tangu jadi .Seneta huyo wa zamani wa Machakos amechekelea kwa bezo mwafaka wa ushirikiano kati ya Kalonzo na Uhuru akisema hautabadilisha chochote .
“ Anafikiria [Kalonzo] Uhuru atamuachia kiti hicho. Hakuna uongozi wa kurithi Kenya ,wakenya wataamua mkondo wanaotaka wenyewe’ Muthama amesema
Ameongeza kwama Ngilu hunda anatuia njama yake dhidi ya kalonzo ili kusalia uongozinikwa kumkaribia Kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa sababu anafahamu kwamba hali imekuwa moto Kitui .
“Ngilu anatafuta njia za kumkaribia Raila ili aweze kupata nafasi ya uongozi’
Muthama amesema atamuunga mkono DP Ruto na watamfuata endapo atasalia Jubilee au ataondoka ili kuanzisha chama kingine .
Mwanasiasa huyo amesema hakuna anayeweza kutetea maslahi ya Ukambani kati ya Kalonzo na Ngilu
"Ngilu hawezi kuongoza muungano thabiti .Mtu anayeweza kufanya hivyo kuiongoza Ukambani ni Kivutha’ amesema
Kivutha ametangaza kwamba atawania urais mwaka wa 2022 hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuanza kujadiliana na wengine kuhusu uwezekano wa kuunda muungano wa kisiasa .