Nguzo tisa muhimu zilizoangaziwa Kwenye BBI

BBI State House-compressed
BBI State House-compressed
Jopo liliojukumiwa kukusanya maoni na kuandika mapendezo ya BBI hatimaye limewasilisha ripoti hiyo maalum kwa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika ikulu ya Nairobi Jumanne.

Wananchi wanatarajiwa kupata ripoti hii rasmi Jumatano ambapo Rais atazindua katika kumbi la Bomas.

Miongoni mwa walioalikuwa kuhudhuria uzinduzi wa Bomas ni viongozi wa serikali wakiwemo zaidi ya watu 100 katika kila kaunti nchini.

BBI ilikuwa na lengo maalum ya kushughulikia mambo tisa kuu kwa kile Rais Uhuru na Raila wanasema ni kuleta utangamano na uwiano.

Hii hapa ni masuala tisa makuu yalioangaziwa:

1. Ufisadi

Rais Uhuru pamoja na Raila Odinga walisimama kidete na kuahidi kwamba misimamo yao kisiasa hautatumika kuwakinga mafisadi wanaopatikana.

Kukithiri kwa ufisadi unasemekana kusababishia taifa hili maendeleo duni.

2. Ukosefu wa maadili kitaifa

Kwa sasa Kenya inaathiriwa na ongezeko la siasa ya migawanyiko hususan miongoni mwa kimbari.

Hata hivyo lengo la BBI ni kuleta uwiano, umoja na maridhiano kitaifa.

3.Ugatuzi

Lengo la viongozi hao ni kuimarisha ugatuzi huku wakiahidi kufanya kazi pamoja na maseneta, wawakilishi wa wadi pamoja na magavana.

Aidha, waliahidi kuhakikisha kwamba huduma za kiserikali zinawafikia Wakenya mashinani.

4. Uchaguzi wa Migawanyiko

Kila baada ya miaka mitano, taifa hili hukumbwa na michafuko kutokana na uchaguzi wa kitaifa.

Mzozano kuhusu matokeo ya kura ya urais hugharimu maisha ya watu wengi pamoja uporaji wa mali na hata mifugo.

Lengo la BBI ni kuhakikisha kwamba uchaguzi unaendeshwa kwa njia ya usawa na haki bila mapendeleo.

5.  Usalama

Wakenya wengi kwa sasa wamo hatarini kutokana na mikasa inayosababishwa na matendo yao bali mengine husabaishwa na hali ya anga.

Hivi maajuzi taifa limepoteza zaidi raia 50 kutokana na mporomoko wa ardhi.

Lipo nia ya kukinga majanga kama hayo katika BBI.

6.  Majukumu na haki za Kibanadamu

BBI inatazamwa kuhakikisha kwamba haki zao za kimsingi zinaheshimiwa.

Aidha, Uhuru na Raila wameahidi kuwaongoza wananchi kuwa wanaowajibika.

7.  Kujumuisha Jamii zote

Kwa muda mrefu, jamii zingine zimekuwa zikilalamikia kutojumuishwa katika nyanja nyingi za kitaifa.

Uhuru na Raila wanaendeleza juhudi za kuhakikisha kwamba makabila yote zaidi ya 43 yanajumuishwa katika nyadhifa zote za kitaifa zikiwemo za urais na baraza la mawaziri.

8. Ustawi kwa wote

Katika sehemu nyingi za taifa hili, maendeleo makubwa yanashuhudiwa huku Kenya ikiwa miongoni mwa mataifa makubwa ya kuwekeza.

Hata hivyo, kuna baadhi ya Wakenya wanaokosa miundo msingi ya kujikimu ikiwemo chakula, mavazi na makaazi.

BBI inatazamiwa kuhakikisha kwamba maendeleo ya maeneo yanaendeshwa bila mapendeleo.

8. Ushindani na Uhasama wa Kimbari

Kwa sasa Kenya imeshuhudia uhasama baina makabila na kusababisha maafa ya hata kulemaza juhudi za maendeleo.

Uhuru na Raila wana lengo la kuhakikisha kwamba  wanasiasa wanashindana kwa uzuri bila kuleta uhasama wa kikabila.