Ni gumzo mtaani. Mithika Linturi na Kitany wana majumba ya kifahari kweli

Mgogoro wa mahusiano kati ya Seneta wa Meru Mithika Linturi na mkewe Kitany umezagaa katika mitandao ya kijamii na kugongwa vichwa vya habari. Hii ni baada ya Kitany kumwaga mtama katika mahakama ya Milimani kuhusu masaibu aliyoyapata katika ndoa hii.

Soma hapa:

Kitany anahoji kuwa Mithika ni mmewe na ana haki ya kupata mgao wa hela na mali wanayomiliki. Seneta Linturi anasisitiza kuwa hajawahi kuwa katika ndoa na Marianne.

Wanandoa hawa walikuwa wanaishi katika majumba ya kifahari kabla uhusiano wao kuvurugika. Tazama baadhi ya picha hapa:

Marianne Kitany ameiambia mahakama ya Milimani kwamba aliamua kusitisha ndoa yake kwa seneta Mithika Linturi  baada ya kupata picha za ponografia katika simu ya mkononi ya seneta huyo. Katika siku yake ya tatu ya kutoa ushahidi kwenye kesi yao ya kutalakiana  Kitani amesema alifaulu kupiga jicho katika simu ya Linturi na kugundua kwamba kuna mwanamke aliyekuwa akimtumia picha za ponografia .

Soma hapa:

Ameongeza kwamba seneta huyo alimnyima haki yake ya tendo la ndoa  na kumfanya kutaka talaka baada ya kugundua kwamba alikuwa na mpenzi wa pembeni.Kitany    amesema yaya mmoja huko Metu alimwambia kwamba Linturi alikuwa akiwaleta wanawake katika nyumba .