Ni kama Movie: Jinsi Gavana Waititu na washirika wake walivyofonza Milioni 25.5

Ufichuzi umeibuka kuhusu jinsi Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na washirika wake walivyotumia njia za kijanja kuiba zaidi ya shilingi milioni 25.6  walizolipwa kama hongo  na wanakandarasi waliopewa zabuni za ujenzi na ukarabati wa barabara katika kaunti ya Kiambu .Stakabadhi zilizotarayarishwa na Tume ya EACC  zinaonyesha kwamba fedha hizo zilihamishwa kwa kiasi kidogo kidogo  ili kupiku mfumo wa benki wa kugundua mbinu za utakatishaji fedha .

Waititu  ameshtakiwa kwa kunufaika kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja na fedha zilizopatikana kwa njia isio halali kupiotia malipo yaliyopewa  Testimony Enterprises  kwa kandarasi zilizotolewa kwa kampuni hiyo na serikali ya kaunti .

Jitihada za kufuata mkondo uliotumiwa kuzihamisha fedha hizo umewafikisha wachunguzi hadi katika biashara zinazohusiana na Waititu  na shilingi milioni 221.5 za sehemu ya kandarasi yenye thamani ya shilingi milioni 588 tayari zimebainika kulipwa kwa kampuni hizo za Waititu .Ili kupata undani wa  njama hiyo ya wizi wa mamilioni ya pesa za kaunti ya Kiambu jipe nakala ya Gazeti la The Star  Alhamisi .