Ni kama Movie! Mama Diamond amzuia Tanasha kuondoka TZ na mjukuu wake Naseeb Junior

Dianmond-Tanasha-break-up
Dianmond-Tanasha-break-up
Sarakasi imezuka  na sasa filamu ipo huko bongo baada ya msanii Diamond Platinumz  na mpenzi wake Tanasha Donna kutengana .

Uvumi unazagaa kwamba Tanasha alipata habari kwamba  Simba alikuwa yungali na tabia za kulala na wanawake wengine nje ya uhusiano wao na hata akathibitisha . Katika posti ya hasira  Tanasha amemtaja Diamond kama ‘shetani’ na mtu ambaye hana utu ndani yake . Tazama .

Baada ya hapo  alifungasha virago vyake na alikuwa akipanga  kuondoka . inaibuka kwamba mamake Diamond  Sandra  hakumtaka Tanasha aondoke akiwa na mtoto wa Diamond  Naseeb Junior .

Udaku kutoka Tanzania waarifu kwamba palitokea kizaazaa kati ya mama Dangote na Tanasha kuhusu mtoto huyo mwenye umri wa miezi mine . Aliandika baadaye katika mtandao

“TIME TO SAY GOODBYE & GOD BLESS YOU ALL.”

Tanasha kwa sasa yuko Nairobi na haijulikani endapo atawahi kusafiri tena kurudi Tanzania