Ni kama torture! Harusi na honeymoon zilizoishia katika quarantine

honeymoon
honeymoon
Wakati unapopanga harusi na fungate, matumaini huwa mengi na mpango  wa awali huwa kujivinjari na kutengeza kumbukumbu za kudumu maisha yenu yote . Francis Mwenda na mkewe  Rosemary hata hivyo wamepitia mazito ambayo wiki chache zilizopita hawakuwahi kufikiria watajipata ndani .

Wiki moja iliyopita  waliabiri ndege ya Emirates  kutoka ubao wakirejea Kenya  wakilenga kupata mapumziko kisha warejee kazini Jumatatu iliyofuata baada ya siku nane za kuzuru maeneo mbalimbali katika Milki hiyo ya kiarabu wakati wa fungate yao . Lakini saa  kadhaa baada ya kutua Kenya, walijipata wamefungiwa katika vyumba tofauti katika  chuo kikuu cha Kenyatta. Baada ya kutembelea vivutio kadhaa Dubai na Abu Dhabi, makao yao mapya yalikuwa kama ndoto mbaya- Vitu ambavyo unatazama tu katika filamu za kuogpofya-horror.

Wakati wa kupewa chakula, wahudumu wanakiacha chakula katika eneo moja kisha wanakuja mmoja mmoja kuchukua chakula, wakati huo wote waloleta chakula wakiwa wametoweka! Wanachosikia tu ni ukemi mtu akisema ‘Chakula’  na kila mmoja anaanza kufika ili kukichukua chakula chake. Mwenda hata hivyo ana bahati ya kuweza kukutana na mkewe nje  kwa sababu taasisi hiyo ina nafasi kubwa .

Wakati mwingine tunatafta kumbukumbu nzuri za kutuunganisha –lakini nyakati kama hizi ,kumbukumbu zozote za kutupitishia magumu zitafanya kazi .