Iwapo unatumia teksi basi hakikisha kwamba ni wewe na dreva wa teksi pekee yenu .
Dhamira ni kuzuia usambaaji wa virusi vya corona. Serikali imepiga marufuku usafiri wa zaidi ya watu watatu katika gari la kuwabeba watu watano. Gari la kuwabeba watu 7 sasa litawabeba watu watatu akiwemo dereva .
Hatua hizo kali ni miongoni kwa zilizotangazwa na waziri wa Afya Mutahi Kagwe na kuwekwa katika gazeti rasmi la serikali ili kuzuia kusambaa virusi vya corona
Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema kwamba arifa hiyo ya gazeti rasmi la serikali sasa ni sharia na polisi wanafaa kuwakamatwa wanaokiuka agizo hilo. Msemaji wa polisi Charles Owino amesema amesema maafisa wa huduma ya kitaifa ya polisi wanafaa kuanza kutekeleza sheria hiyo mara moja .