Ni mara ngapi unaongea na baby mama wako? Diana amuuliza Bahati

Screen-Shot-2018-04-26-at-7.42.46-AM-348x216
Screen-Shot-2018-04-26-at-7.42.46-AM-348x216
Msanii wa nyimbo za injili Bahati na mkewe Diana Marua wamekuwa wakipost filamu mbali mbali katika mitandao yao ya kijamii huku wakiulizana maswali na kuyajibu.

Jana Diana alimuuliza Bahati ni mara ngapi yeye huzungumza na baby mama wake Yvette Obura.

"Kwa muda mrefu sasa hatujakuwa na mawasiliano kwa sababu ya mambo mawili matatu hivi, lakini mwisho wa mwaka wa 2019

Niliona ni muhimu kuwasiliana na baby mama wangu kwa maana kilicho muhimu ni mtoto wangu Mueni." Alieleza Bahati.

Aliendelea kusema kuwa hapo awali alikuwa anampigia nyanya wa Mueni yaani mama yake Yvette ili azungumze na mwanawe.

Lakini muda ulipozidi kusonga mawasiliano hayo yalianza kudidimia.

" Huwa naongea na baby mama wangu wakati mtoto wangu anataka kuzungumza na mimi ama wakati mimi mwenyewe nataka kuzungumza na yeye kwa hivyo sina wakati maalum." Alijibu Bahati.

Aliongeza,

"Kwa wakati mwingine huwa nataka kujua vile anaendelea na masomo yake, ili nijue kama karo ya shule ambayo nalipa inatumika mzuri au la.

Unajua mimi ni mtu alikula karo ya mzungu katika shule ya watoto yatima, kwa hivo sitaki mtoto wangu akule karo ya shule." Alisema Bahati.

Diana alimuuliza ni mara ngapi wao huongea kwa siku.

"Wakati mwanangu anataka kuzungumza na mimi, kwa hivo ni mara moja kwa siku." Bahati Alimwambia.

"Unafikiria ni muhimu nijuwe kuwa wewe huongea naye?

"Hapana sidhani mna haja ya kujua." Alisema.

Mashabiki walitoa maoni yao kuhusu suala hili,

Esther Ngari Tell him to buy Mueni a phone, period!

Nancie Lloyds Diana I think you should be told every time, she has been called. Aki baby Mama’s can be very irritating chunga asikugeuzie serikali in the name of checking on mueni then don’t meet up with her. I feel it’s better make mbali na each other… If it gets to meeting up ikue kwa restaurant sio home kwako .

Elsie Snaider out of Solomon’s wisdom I think dee deserves to know because she’s now your wife

Emmiliana Msagath It’s important for Diana to know

Monica Wanjiku Yes I should know Dee in fact he should call her when ur both 2gether