Ni nani mshambulizi bora katika ligi ya Uingereza?

Ligi ya Uingereza ambayo inajulikana sana barani Ulaya kwa kukuza washambulizi bora duniani umeendelea kushuhudia ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji mbalimbali wanaochezea klabu tofauti.

Katika msimu huu wa mwaka 2019/2020, washambulizi wengine wapya wamejitokeza na kuthibitisha makali yao kwa kutikisa nyavu zaidi ya mara tano.

Wachezaji hao ni Tammy Abraham na Teemu Pukki ambao wanachezea klabu ya Chelsea na Norwich.

 Ligi hiyo ya Uingereza bado haujakamilika lakini wafuatao ni wachezaji ambao wamefunga mabao zaidi tangu msimu huu uanze;

Jamie Vardy

Mshambulizi huyu anachezea klabu ya Leicester na vile vile ameweza kufunga mabao 17.

Sergio Kun Aguero

Mshambulizi huyu ambaye ametajika kwa muda wa karibu miaka tano katika ligi ya Uingereza kwa makali yake anaichezea klabu ya Manchester City.

Kwa sasa anaongoza katika orodha hilo la wachezaji ambao wamefunga bao huku akiwa ametikisa nyavu mara tisa.

Tammy Abraham

Ni mshambulizi katika klabu ya Chelsea. Vile vile ameweza kufunga mabao kumi na moja msimu huu.

Pierre Emerick Aubameyang

Anachezea klabu ya Arsenal. kwa sasa Aubameyang ameweza kupachika mabao 11.

Raheem Sterling

Muingereza huyu anachezea klabu ya ManCity na ameweza kutikisa nyavu mara tisa.