Tasnia ya burudani kwa sasa imejaa wanaume na wanawake wengi wanaojituma katika haso za kila siku za kuwapatia watu burudani kwa kutumia sahani za santuri. Kuna ma-deejay wanaofanya kazi kwenye redio, runinga, vilabu na pia kanisani na maeneo mengine ya burudani au tamasha.
Soma hapa:
Hali kadhalika kuna wale wafanyabiashara wamechukua kipaji hiki kama biashara na kufungua shule za kutoa mafunzo kwa vijana wanaotamani kuwa ma-deejay.
Kulikuwepo na dhana kuwa tasnia hii haihitaji masomo shuleni ila kuna baadhi ya ma-deejay kama Creme Dela Creme, Dj Juan, Dj Mo na Sadiq ambao wametokea na kuuzima mtazamo huu.
Pata Uhondo hapa:
Japo huwa tunafurahi sana tunapopata madini mazuri ya miziki inayochezwa na wanasanaa hawa, kuna baadhi ya tabia wanazofanya hazivutii kabisa:
- Kufanya mauzo au kujitangaza katikati ya ngoma - Ghafla utakuwa unasikiliza muziki afu deejay ashtukize kwa kutupia pale majina yake kwenye mitandao ya kijamii
- Kutuma salamu kwa wapenzi wao na wanadada hususan kwenye vilabu. Utaskia, “Shiro was Githu 44, umesalimiwa” ama “A gyal dem, Beyonce wa Ungwaro niaje?”.
- Visauti vya kurembesha ngoma vinachombezwa katikati kama: ‘you’re chilling with best DJ in Kenya’, ‘come back selecta’, ‘mbrrrrrcha, awuoooh, thitima’ and ‘your girlfriend’s favourite DJ’.
- Deejay kuimba muziki unapocheza- Kazi ya deejay ni kuucheza muziki mashabiki wausikilize ila sio kuimba. Mashabikib wakitaka kuimbiwa wataenda Kosewe au ata kwenye matamasha yanayofanywa na bendi na kutazama na kusikiliza .