Ni ukweli tunapanga kitu na Rais Kenyatta - Isaac Ruto asema

unnamed (7)
unnamed (7)
Baada ya taarifa kuvuma katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kikao kilichomshirikisha rais Kenyatta na gavana wa zamani wa Bomet Isaac Ruto kuibuka, ni wazi kuwa taarifa hizo zilikuwa za ukweli. Hii ni baada ya Ruto kukiri kuwa amekuwa kwa mazungumzo na kiongozi wa taifa na wanapania kushirikiana ili kufanya kazi pamoja.

Ruto ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Mashinani amesema alikutana na rais ili kukubaliana ni jinsi vyama hivyo viwili vitakavyofanya kazi pamoja.

“The Party Leader Hon Isaac Rutto met with the President H.E Uhuru Kenyatta and agreed in principle that the two parties work together in the interest of peace, cohesion and development in the country,” Amesema Kiprotich Samoei katika taarifa iliypotumwa kwa vyombo vya habari,

Ruto alichukuliwa na ndege kutoka nyumbani kwake Bomet kukutana na rais Kenyatta licha ya chama chake kukana taarifa hizo.

Aidha, Jumatano chama hicho cha CCM kulisema kuwa kulikuwepo na mkutano baina ya viongozi hao wawili haswa baina ya chama chake na Jubilee.

Ruto was picked by a chopper from his rural home in Bomet for a meeting with the President but immediately after the news leaked, CCM came out to strongly deny.

“As you may recall, Isaac Ruto was the first Nasa principal to do a handshake with the President before the repeat election when he joined him at a campaign rally at Kapkatet on 8 September 2017 and endorsed his re-election and pledged to work with the President,” CCM imesema

Cha kushangaza ni kuwa, kiongozi wa CCM Isaac Ruto ni rafiki mkubwa zaidi wa Gideon Moi kiongozi wa chama cha Kanu. Mkutano baina ya Ruto na Kenyatta umeibua hisia kali miongoni mwa wananchi ikidaiwa kuwa huenda rais Kenyatta anataka kumtumia kama njia ya kumpiga vita kisiasa naibu ukanda wa Rift Valley.