Ni vyema kumaliza uhusiano kwa njia ya amani’ Hamisa Mobetto ashauri

Suala  la kuendelea na uhasama baada ya kutengana na mtu lipo katika fikra za Hamisa Mobetto na ameamua kutoa ushauri wake .

Mrembo huyo wa video za muziki ametuma ujumbe ficge akijaribu kueleza umuhimu wa mtu na mpenziwe wa zamani kundelea kuwa marafiki .

Mwezi machi Hamisa na Diamond  walionekana  kujaribu kurejesha  penzi lao  na hata msanii huyo alisema anajua Haisa humtamani . Hamisa alikuwa akuiucheza wimbo wa Diamond ‘Jeje’  na Chibu alisema alifahamu kuna alichotaka mwanadda huyo

Aliandika ujumbe huu ambao Wema Sepetu alikubaliana nao ;

Kuna wakati itabidi uachane na mtu uliyekuwa unampenda sana na ulidhani utakuwa naye kwa muda mreeefu.

Kuna wakati katika maisha utalazimika kuachana na watu, ofisi…. n.k.

Ukifika wakati huu kuna mambo ya kuzingatia.

Moja, sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao.

Unaweza kuachana kwa HESHIMA na UTULIVU.

Kumbuka kuachana sio VITA, mnaweza kuachana na maisha yakaendelea.

Aliongeza

Sio lazima uwageuze ADUI wale unaowaacha au wanaokuacha.

Maisha yana majira na kila mtu anatakiwa kuwa mahali fulani kwenye majira tofauti.

Mbili, pokea maumivu na yakubali. Haitasaidia kutokubali uhalisia.

Kama mtu ameamua kuondoka, hakuna namna.

Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa hatua inayofuata.

Tatu, usijilazimishe kuonyesha ubaya wa unayeachana naye.

Kumbuka mafanikio ya UNAKOKWENDA hayajabebwa na watu kujua ubaya wa UNAYEACHANA naye bali yamebebwa katika DHAMIRA SAFI ya UNACHOKWENDA KUFANYA.

Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unayeachana naye.

Wengi walijaribu kuutafsiri ujumbe huo lakini ni gayana kwamba umeelekezewa Diamond na tofaui zake na baadhi ya wanawake aliozaa nao watoto